Stars yapangwa pazuri CHAN

KENYA; NAIROBI, DROO ya makundi ya michuano ya Afrika kwa Wachezaji wa Ligi za Ndani (CHAN), imepangwa usiku huu huku Tanzania ikiwa Kundi B pamoja na nchi za Madagascar, Mauritania, Jamhuri ya Afrika ya Kati na Burkinafaso.

Kundi hilo ukiacha Burkina Faso, timu nyingine hazina majina makubwa katika soka la Afrika, ingawa Madagascar miaka ya karibuni imeonesha kiwango kikubwa katika michuano ya Mataifa ya Afrika (Afcon).

Michuano ya CHAN inayotarajiwa kufanyika Agosti mwaka huu itaandaliwa kwa pamoja na Tanzania, Uganda na Kenya, ambapo Kenya ipo Kundi A na nchi za Morocco, Angola, Zambia na Jamhuri ya KIdemokrasia ya Congo (DRC), likionekana kama Kundi la Kifo.

Makundi kamili ni kama ifuatavyo:

  • Kundi A: Kenya, Morocco, Angola, DR Congo, Zambia
  • Kundi B: Tanzania, Madagascar, Mauritania, Burkina Faso, Jamhuri ya Afrika ya Kati
  • Kundi C: Uganda, Niger, Guinea, Q2, Q1,
  • Kundi D: Senegal, Congo, Sudan, Nigeria,

Habari Zifananazo

Back to top button