CHUO Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kupitia Shule Kuu ya Elimu kimejipanga vyema kuhakikisha miundombinu ya ufundishaji inakuwa rafiki kwa wanafunzi mkondo wa elimu amali katika Shule ya Sekondari Mafiga ulioanza kutekelezwa Januari mwaka huu ili wanawajengea uwezo wanafunzi hao kujitegemea baada ya masomo.
Amidi Mkuu wa Shule Kuu ya Elimu SUA, Dk Jamal Jumanne amesema hayo alipomwakilisha Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu hicho kwenye mahafali ya 15 ya wanafunzi wa kidato cha nne wa shule hiyo.
Dk Jumanne akimwakilisha Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu hicho katika mahafali hayo katika shule hiyo ambayo SUA ni mbia katika kusimamia mwendeshaji wa elimu ya amali .
Amidi Mkuu wa Shule Kuu ya Elimu SUA ,amesema lengo kuu la Elimu ya Amali ni kukuza ujuzi unaoweza kutumika moja kwa moja katika mazingira halisi ya kazi au maisha.
Naye Amidi Shule Kuu Elimu wa Chuo Kikuu SUA ,Dk Benedicto Msamgya amesema Chuo hicho kinaipongeza Serikali kupitia mitaala mipya ya elimu amali.
Dk Msangya ambaye pia ni Mratibu wa Shule ya Sekondari Mafiga kutoka chuo hicho amesema SUA ina vitengo vingi vikiwa vya elimu kuna shule ya elimu ambayo inaaandaa walimu a wa masomo mbalimbali kwa ajili ya kufundisha masomo ya sayansi .
Amesema chuo hicho kiliomba kupatiwa shule ya mazoezi ambao wanafunzi wao wa elimu baada ya kupata mafunzo waweze kufanya mazoezi ya ufundishaji na kwamba waliomba shule kadhaa lakini Serikali ikawapatia Sekondari ya Mafiga kwa ajili ya wanafunzi wao .