CHUO Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kipo tayari kushirikiana na Tume ya Rais ya Kuangalia Jinsi na Kuboresha Taasisi za Haki Jinai ili kutoa elimu inayohusiana na haki jinai ili iweze kuwafanya wananchi washirikishwe vizuri na Vyombo vya Haki Jinai.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu hicho, Profesa Raphael Chibunda amesema hayo kwa wajumbe wa Tume hiyo wakiongozwa na Mjumbe Mkuu wa Jeshi la Polisi Mstaafu ,Balozi Ernest Mangu, wakati wa mhadhara na wanajumuiya wa Chuo Kikuu hicho.
Balozi Mangu aliambatana na wajumbe wenzake ambao ni Katibu Mkuu ( Utumishi) ,Mstaafu , Dk Laurean Ndumbaro pamoja na Mkurugenzi wa Utafiti katika Chuo Kikuu cha Zanzibar (SUZA), na Rais Mstaafu wa Chama cha Wanasheria Zanzibar , Dk Yahya Khamisi Hamad.
Tume ya Haki Jinai ina wajumbe tisa wakiongozwa na Mwenyekiti wake Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Othman Chande, na Makamu wake Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu , Balozi Ombeni Sefue .
Profesa Chibunda amesema ,Chuo kikuu kiliona ni umuhimu kuialika Tume hiyo ili kuongea na wafanyakazi na jamii ya wanachuo waweze kusikia mapendekezo ya tume hiyo , kwa kuwa wao ni sehemu ya jamii na wanufaika wa elimu hiyo.
Amesema ,Taasisi za Elimu ya Juu ni watumiaji wa Vyombo vya Haki Jinai ,na wanayo matumiani ya kwamba sheria zitabadikika kulingana na mapendekezo yaliyowasilishwa na Tume hiyo.
“SUA tupo tayari kushirikiana na Tume na serikali katika kutoa elimu inayohusiana na haki jinai katika nchi yetu ili kuweza kuwafanya wananchi washirikishwe vizuri na vyombo vyetu vya haki jinai “ amesema Profesa Chibunda
Profesa Chibunda amesema ,mafanikio hayo yanaweze kuchochewa zaidi endapo mtizamo na fikra za watendaji katika vyombo vya haki jinai zitabadilika kama ilivyopendekeza tume hiyo ,na kuifanya jamii na taasisi za elimu ya juu kuwa wanufaika.
Comments are closed.