Sudan yalaani vikwazo vya Marekani dhidi ya Abdel Fattah

SUDAN : WIZARA ya Mambo ya Nje ya Sudan inayoungwa mkono na jeshi imelaani vikwazo vilivyotangazwa na Marekani dhidi ya Mkuu wa Jeshi, Abdel Fattah al-Burhan, ikisema kuwa hatua hiyo haina msingi wa haki na uwazi.

Katika taarifa yake, wizara hiyo imesema vikwazo hivyo vinachangia mkanganyiko katika mzozo unaoendelea, ambao umeingia mwezi wa 21 wa vita kati ya jeshi la Sudan na vikosi vya RSF.

Wizara imesisitiza kuwa Burhan anawatetea raia wa Sudan dhidi ya kile kilichotajwa kama njama ya mauaji ya kimbari. SOMA: Mapigano yauwa watu 100 Sudan

Wizara ya Fedha ya Marekani ilitangaza vikwazo dhidi ya Burhan, na kulishutumu jeshi la Sudan kwa kushambulia shule, masoko, na hospitali, na pia kutumia chakula kama silaha ya vita.

Hatua hii inajiri wiki moja baada ya Marekani kumuwekea vikwazo kiongozi wa RSF, Mohamed Hamdan Daglo, na kulishutumu kundi lake kwa kufanya mauaji ya halaiki.

Tangu kuanza kwa mzozo huo mwezi Aprili 2023, pande zote mbili zimekuwa zikishutumiwa kwa kuwalenga raia na kushambulia maeneo ya makazi kwa makombora.

Habari Zifananazo

Back to top button