Taasisi yakabidhi madarasa shule ya Mzimuni

ARUSHA: TAASISI ya Vijana ya Ndoto Action imekabidhi jumla ya madarasa 10 yenye thamani ya Sh milioni 700 kwa Shule ya Msingi Mzimuni, iliyopo katika kata ya Nduruma Halmashauri ya Wilaya ya Arusha ikiwa ni sehemu ya mchango wake katika kuboresha sekta ya elimu.
Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano hayo yamefanyika katika shule hiyo, Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Arusha ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Uratibu na Mipango, Anna Urio, alishukuru taasisi ya Ndoto Action kwa mchango huo mkubwa unaosaidia kupunguza msongamano wa wanafunzi madarasani na kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji.

Amesema serikali itaitunza miundombinu hiyo iliyojengwa na taasisi hiyo ili kuhakikisha kuwa inasaidia jamiii kama ilivyokusudiwa na kutoa wito kwa wadau wa maendeleo kuendelea kushirikiana na serikali katika ujenzi wa miradi mbalimbali
“Uwepo wa madarasa haya utasaidia ufundishaji na ujifunzaji kwa walimu na wanafunzi sanjari utulivu wa kusoma darasani kwa wanafunzi kutokana na mazingira yaliyopo, tunashukuru taasisi hii ya mfano katika maendeleo ya sekta ya elimu”
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Vijana ya Ndoto Action, Hussein Salim amesema ujenzi wa madarasa hayo utasaidia kutatua kero mbalimbali ambayo zimekuwa zikiikabili shule hiyo ikiwemo ukosefu wa madarasa pamoja na wingi wa wanafunzi madarasani.

Amesema taasisi hiyo imekuwa ikitekeleza miradi mingine mbalimbali ya kielimu katika shule hiyo ikiwemo miradi ya mashamba yatakayosaidia upatikanaji wa chakula na lishe bora pamoja na matenki zaidi ya 30 ambayo yatawezesha uvunaji wa maji nyakati za mvua.




Thank you for taking your time to write this story and for actually attending the handover event.