Taasisi za umma Tandahimba zahimizwa nishati safi

TANDAHIMBA: KIONGOZI wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Wazo Mwang’onda amezitaka taasisi za umma kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba mkoani Mtwara kuhakikisha zinatumia nishati safi ya kupikia ili kuunga mkono juhudi za serikali juu ya matumizi ya nishati.

Ametoa agizo hilo leo Mei 6, 2026 wakati Mwenge wa Uhuru mwaka 2026 ulipopokelewa kwenye kijiji cha Miuta wilayani humo ukitokea Halmashauri ya Mji Nanyamba.

Aidha mwenye umepitia miradi mbalimbali ya maendeleo 7 yenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 800 ikiwemo huo wa nishati safi ya kupikia.

Mwenge wa Uhuru ukiwa wilayani humo umekimbizwa umbali wa kilomita 116 ambapo katika miradi hiyo 7 miradi 5 kuwekewa mawe ya msingi, mradi 1 kukagua na mwingine kuona na kukagua.

Miradi hiyo iliyopitiwa na Mwenge ikiwemo huo wa nishati safi, mradi wa maji lyenje uliyopo kijiji cha lyenje, Shule ya Msingi Shikizi mnauke kwenye kata Nanhyanga na mingine.

Kiongozi huyo wa Mbio za Mwenge amesema mwenge umeridhia kuzindua mradi huo na kuisisitiza jamii kuendelea kuhamasika na matumizi ya nishati hiyo ili kutunza mazingira na kuondokana na matumizi ya kuni na mkaa.

“Nimpongeze Rais kwa kubariki nishati hii na kuifikisha mashuleni na sasa tunaanza kuitumia pamoja na kuhifadhi mazingira,”amesema Wazo.

Ameongeza kuwa: “Niziagiza taasisi zote za umma kutumia nishati safi ya gesi ambayo leo imezinduliwa ili kuendelea kutunza mazingira,”amesisitiza Wazo

Akisoma taarifa kuhusu mradi huo, Mkuu wa Shule hiyo ya Sekondari Kitama Consolata Nchimbi amesema uwepo wa mradi huo wanafunzi hawatapoteza muda na nguvu ya kutafuta kuni.

“Matumizi wa nishati safi yatakuwa ni shamba darasa kwa wazazi na wananchi watakaofika shuleni hapa pia ni matumaini yetu kuwa kupitia mradi huu tutaunga mkono juhudi wa Rais Samia Suluhu Hassan”

Habari Zifananazo

One Comment

  1. I tried a similar approach with rosemary last week, but the flavor was a bit too strong for my liking. Maybe a lighter hand is needed next time, or a different herb entirely. What do you think about marjoram as a substitute here?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button