Tabora United: Tumemalizana vizuri na Goran

MSEMAJI wa Tabora United Christina Mwagala ameweka wazi kwamba hawadaiwi na aliyekuwa kocha wao Goran Copunovic waliyesitisha mkataba wake kutokana na matokeo mabaya.

Kocha Goran aliyewahi pia kuifundisha timu ya Simba ya Dar es Salaam, hakuwa na mwendelezo mzuri tangu alipojiunga na kikosi hicho mwanzoni mwa msimu huu.

“Tumejifunza kutokana na makosa yaliyowahi kutokea tukawa tunadaiwa baada ya kusitisha mikataba ya wachezaji. Kwa kocha Goran tumeachana naye vizuri na hatudaiani tumemalizana vizuri,” amesema Mwagala.

Habari Zifananazo

Back to top button