TIMU ya Taifa ya soka “Taifa Stars” leo inashuka dimbani katika mchezo wa kufuzu fainali za Kombe la Mataifa Afrika (AFCON) dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-DR Congo.
Mchezo huo wa kundi H utafanyika kwenye uwanja wa Des Martys uliopo mji mkuu wa DR Congo, Kinshasa.
SOMA: Taifa Stars yafuzu Afcon 2023
DR Congo inaongoza kundi hilo ikiwa na pointi 6 baada ya michezo 2 ikifuatiwa na Tanzania pointi 4, Ethiopia pointi 1 na ya mwisho ni Guinea ambayo na haina pointi.
Michezo mingine ya kufuzu AFCON inayopigwa leo ni kama ifuatavyo:
KUNDI E:
Algeria vs Togo
KUNDI F
Ghana vs Sudan
KUNDI J
Burkina Faso vs Burundi