Taifa Stars yaanza kibabe safari ya Kombe la Dunia
MOROCCO: Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars imeanza vyema kampeni ya kuisaka tiketi ya kucheza Michuano ya kombe la Dunia mwaka 2026 kwa kuitandika Niger 1-0 katika mchezo uliopigwa nchini Morocco.
Bao la Stars limefungwa na Charles M’mombwa katika kipindi cha pili cha mchezo huo, matokeo hayo yameifanya Stars kuandikisha alama 3 za kwanza kwenye kundi E.
Mchezo unaofuata utapigwa Novemba 21 dhidi ya Morocco katika Uwanja wa Benjamini Mkapa kuanzia saa nne usiku.