Taifa Stars yaifuata Uganda

KIKOSI cha timu ya soka ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, kimeondoka alfajiri ya leo kuelekea nchini Misri kwa ajili ya mchezo wa kufuzu mashindano ya AFCON dhidi ya Uganda utakaopigwa Jiji la Ismailia Machi 24, 2023.

Katika taarifa iliyotolewa leo Machi 19, Shirikisho la Soka Mpira wa Miguu nchiniĀ  (TFF) limeeleza kuwa wachezaji wanaocheza nje ya Tanzania watajiunga na kikosi hicho moja kwa moja nchini Misri.

Aidha wachezaji wa Yanga ambao leo wataitumikia klabu yao katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Monastir wao watasafiri kesho kuelekea nchini Misri kwa mujibu wa tarifa hiyo.

Baada ya mchezo huo, Taifa Stars itarejea nchini Machi 25, kujiandaa na mchezo wa marudiano utakaochezwa Machi 28 katika Uwanja wa Mkapa Dar es Salaam

Habari Zifananazo

Back to top button