Taifa Stars yakwamia 16 bora AFCON

MOROCCO; TIMU ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imeshindwa kuingia robo fainali ya michuano ya Mataifa ya Afrika baada ya kufungwa bao 1-0 na wenyeji Morocco katika mchezo wa hatua ya 16 bora usiku huu wa Janauri 04, 2026.
Hata hivyo wachezaji wa Taifa Stars walimlalamikia kwa kiasi kikubwa mwamuzi Boubou Traoré, wakionekana kupinga kwa kiasi kikubwa maamuzi yake ikiwemo madai ya kuwanyima penalti dakika za mwishoni za mchezo huo.

Morocco walimaliza kileleni mwa Kundi A wakiwa na pointi saba, huku Taifa Stars wakiwa nafasi ya tatu katika Kundi C ikiwa na pointi mbili, wakiibuka kati ya timu zilizoshika nafasi za washindwa watatu bora.
Taifa Stars ilifungwa na Nigeria 2-1 katika mchezo wa kwanza, kabla ya kutoka sare ya 1-1 dhidi ya Uganda na Tunisia.

Morocco ‘Simba wa Atlas’ waliichapa Comoro mabao 2-0, sare ya 1-1 na Mali na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Zambia.
Jana Serikali ya Tanzania iliizawadia Taifa Stars kiasi cha Sh milioni 500, kufuatia kufuzu hatua ya 16 Bora katika michuano ya AF CON 2025.




