Takukuru kutoa elimu ya rushwa uchaguzi mitaa

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imesema itatumia mikutano hadhara ya kampeni ya vyama vya siasa katika uchaguzi wa serikali za mitaa kuendesha kampeni na kutoa elimu ya kupambana na rushwa.
Ofisa elimu kwa umma kutoka taasisi hiyo Mkoa Kigoma, Ibrahim Sadiki amesem hayo katika semina ya siku moja kwa waandishi wa habari mkoani humo kuhusu kampeni ya kupinga vitendo vya rushwa kwenye Uchaguzi Mkuu na uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Ofisa elimu kwa umma wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoa Kigoma (TAKUKURU) Ibrahim Sadiki
Sadiki amesema kutumika kwa njia kunatokana na mafanikio makubwa ambayo Takukuru imeyapata katika kuendesha kampeni zake za elimu kwa umma kwa kutumia mpango wa Takukuru Rafiki ambapo walitumia mikutano ya hadhara.
SOMA: Takukuru yabaini harufu ya rushwa uchaguzi mitaa
Mwanasheria Takukuru Mkoa Kigoma Jackson Lyimo
Akizungumza katika semina hiyo Mwanasheria wa Takukuru Kigoma , Jackson Lyimo amesema pamoja na mikutano kuleta mafanikio makubwa katika kupatikanaji wa taarifa za rushwa pia waandishi wa habari wamekuwa na mchango mkubwa katika kuibua vitendo na viashiria mbalimbali vya rushwa mkoani Kigoma.
SOMA: Takukuru yabaini kasoro miradi 171
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Kigoma (KGPC), Jacob Ruvilo amesema semina kama hizo zina manufaa makubwa na kuwapa uelewa mambo mbalimbali lakini kuwafanya Takukuru na waandishi wa habari kufanya kazi pamoja kama timu na kupeana mipaka ya kazi na majukumu yao.