TAKUKURU yaomba ukaguzi mkopo wa halmashauri

MKUU wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Shinyanga, Donasian Kessy ameomba ukaguzi maalum kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi  Mkuu wa Fedha za Serikali (CAG) kwa ajili ya kuchunguza mkopo wa Sh milioni 900 wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.

Mkopo huo walikopa kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi  kwa ajili ya  upimaji wa viwanja 2000.

Kessy amesema hayo leo Mei 25, 2023 alipozungumza na waandishi wa habari wakati akitoa taarifa ya kipindi cha robo ya  tatu ya mwaka wa Fedha 2022/2023.

Kessy amesema walipofanya uchunguzi wa awali walibaini fedha hizo kuwekwa kwenye akaunti tofauti tofauti hivyo wameomba kibali maalum kwa CAG ili kuweza kukamilisha uchunguzi huo.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x