Takukuru yachunguza tuhuma 285 taarifa ya CAG

DAR ES SALAAM; TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), imesema katika kipindi cha mwaka 2023/24, imefanya uchunguzi wa majalada kuhusu tuhuma 285 ambazo zilitokana na taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka 2022/23.

Kauli hiyo imetolewa leo Machi 27, 2025 na Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Crispin Chalamila, wakati wa kukabidhi taarifa ya utendaji kazi ya mwaka 2023/2024 kwa Rais Dk Samia Suluhu Hassan, Ikulu, Dar es Salaam.

“ Kutokana na tuhuma hizo:Tuhuma 145 zilifungwa kwa kukosa ushahidi unaothibitisha vitendo vya rushwa pasipo shaka (beyond reasonable doubt). Tuhuma 140 zilifunguliwa majalada na uchunguzi wake kukamilika ambapo watuhumiwa walifikishwa mahakamani.

“ Katika kesi 140 zilizofunguliwa mahakamani, kesi 55 zimeamuliwa na Jamhuri ilishinda kesi 41. kesi 4 zimeondolewa mahakamani na Kesi 81 zinaendelea kusikilizwa katika hatua mbalimbali,’ amesema Mkurugenzi huyo

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button