TAKUKURU Yaokoa Sh Bilioni 14.5

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imesema imefanikiwa kuokoa shilingi bilioni 14.5 kupitia operesheni mbalimbali za uchunguzi. Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Crispin Chalamila, ameeleza hayo Ikulu, Dar es Salaam, alipokuwa akimkabidhi Rais Samia Suluhu Hassan taarifa ya utendaji kazi wa taasisi hiyo kwa mwaka 2024/2025.

Chalamila amesema kati ya fedha hizo, shilingi bilioni 10.1 ni fedha taslimu zilizowekwa kwenye akaunti za taasisi na idara za serikali, huku shilingi bilioni 4.4 zikihusisha mali na vifaa vilivyodhibitiwa na kurejeshwa katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Amefafanua kuwa fedha hizo zimepatikana katika maeneo mbalimbali, ikiwemo shilingi bilioni 1.2 za ushuru wa huduma uliokuwa haujalipwa kwa halmashauri na kampuni za Mastermind Tobacco Ltd na Beijing Construction Engineering Group Company Ltd.“Kupitia operesheni za TAKUKURU, fedha hizi zililipwa katika halmashauri husika,” alisema.

Aidha, amesema shilingi milioni 770 ni mikopo iliyokuwa imetolewa na Benki ya NBC kwa vyama vya ushirika vinavyolima tumbaku, ambayo awali haikurejeshwa lakini ililipwa baada ya ufuatiliaji wa TAKUKURU. Ameongeza kuwa shilingi milioni 221 zilipatikana kutokana na mauzo ya viwanja katika Halmashauri ya Manispaa ya Kahama, eneo la Nyasubi, ambapo wanunuzi hawakuwa wamelipia viwanja hivyo ipasavyo.

Chalamila amesema taarifa hiyo inahusu kipindi cha Julai 2024 hadi Juni 2025. Amebainisha pia kuwa katika kipindi cha Julai 2025 hadi Februari 2026, TAKUKURU imefanikiwa kuokoa zaidi ya shilingi bilioni 101.8 kupitia operesheni zake mbalimbali. SOMA: CAG: Hati 1,326 zinaridhisha

Kwa upande wa uchunguzi, amesema TAKUKURU ilikamilisha majalada 1,030, yakiwemo 22 ya rushwa kubwa yenye thamani ya shilingi bilioni 210.5. Aidha, uchunguzi huo ulibaini kuwepo kwa mtandao wa kughushi kadi za benki, ambapo zaidi ya shilingi bilioni 147.5 ziliondolewa kwenye akaunti za wateja bila ridhaa yao.“Fedha hizi zililipwa kupitia matumizi ya kadi 1,551 kutoka mataifa 11, zikihusisha makampuni 162 na benki tano hapa nchini,” alisema.

Ameongeza kuwa kadi hizo zilitumika kulipia huduma mbalimbali ikiwemo utalii, usafirishaji, kodi na bima ya afya, huku baadhi ya watuhumiwa wakijihusisha na utakatishaji fedha uliosababisha hasara ya shilingi bilioni 2.6 kwa benki. Kwa mujibu wa Chalamila, jumla ya kampuni 82 za utalii katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Dar es Salaam na Mwanza zilihusika kutumia kadi zilizoghushiwa kinyume cha sheria.

 

 

 

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 12000-16700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
    .
    This is my main concern…………………… http://Www.Cash54.Com

  2. I just came across this amazing way to earn $11,000-$15,000 a month online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
    .
    This is what I do…………………… http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button