AFGHANISTAN: MWAKILISHI wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Roza Otunbayeva amesema Taliban imewakamata waandishi wa habari 256 tangu walipoingia madarakani miaka mitatu iliyopita.
Katika ripoti hiyo,Otunbayeva amesema waandishi wa habari nchini Afghanistan wamekuwa hawana uhuru wa kufanya kazi zao. Soma: Kesi ya Septemba 11 kunguruma wiki ijayo
Hatahivyo,wizara ya mambo ya nje ya Taliban imekanusha taarifa hiyo na kusema hakuna ukweli wowote kuhusu taarifa hiyo na badala yake wamekuwa wakiwalinda waandishi wa habari wakati wote.