Talis bingwa wa jumla kuogelea

DAR ES SALAAM; klabu ya Kuogelea ya Talis imetwaa ubingwa wa jumla michuano ya kuogelea klabu bingwa taifa iliyomalizika leo kwenye bwawa la Kuogelea la Shule ya Kimataifa ya Tanganyika IST.

Katika shindano hilo lililoshirikisha wachezaji zaidi ya 100 kutoka klabu mbalimbali washindi walikabidhiwa vikombe na medali.

Talis walishinda baada ya kufikisha pointi 456, nafasi ya pili ikishikiliwa na Dar Swim iliyofikisha pointi 354 na nafasi ya tatu ni Ripride iliyopata pointi 89

Mwenyekiti wa Chama cha Kuogelea Tanzania (TSA), David Mwasyoge amesema wamefarijika kuona wachezaji wakijitahidi kwa kufanya vizuri.

“Niwapongeze wachezaji na makocha kwa kazi kubwa,mmeonesha ushindani wa hali ya juu. Pia, niwapongeze wale waliovunja rekodi mmejitahidi “amesema.

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button