Tamasha la FINTECH kuibua fursa za uwekezaji wa kiteknolojia

TAMASHA la Fintech la teknolojia ya kifedha Ukanda wa Afrika Mashariki limetajwa kuwa tamasha kubwa zaidi katika ukanda huo.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Eastern Star Consulting Group, Deogratius Kilawe ameeleza hayo wakati akifungua tamasha hilo lililowakutanisha wakali wa teknolojia wa fedha kutoka nchi zaudi ya 17 duniani.
Tamasha hilo lilianza Juni 13, katika ukumbi wa Julius Nyerere International Convention Center (JNICC).
Katika tamasha hilo, Jumuiya ya FINTECH iliungana na wawakilishi hao wa mataifa 17 katika kujadili fursa mbalimbali zinazosaidia kukuza teknolojia ya kifedha.
Aidha, tamasha hilo pia lilijadili namna mbalimbali za kuinua uchumi kwa njia ya teknolojia.