Pamba Fc wazindua tawi sengerema

MWANZA: ZIKIWA  zimebaki siku chache kabla ya siku inayosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka Jijini Mwanza kuelekea tamasha la Pamba day

Kampeni ya  Pamba  bay imezidi kuwabamba mashabiki baada ya kufunguliwa kwa  tawi jipya la mashabiki wa timu ya Pamba Jiji Fc katika Halmashauri ya Buchosa Wilayani Sengerema.

Tawi hilo la mashabiki wa Pamba Jiji FC limefunguliwa Augasti mosi mwaka huu na na katibu tarafa wa kata ya Kahunda,Joseph Kapunda kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Senyi Ngaga.

Advertisement

“Tunawajibu wa kushikamana kwa vitendo kuiunga mkono timu yetu ya Pamba Jiji Fc ambayo mbali na burudani imekuja kuinua uchumi wa mkoa wetu,”amesema Kapunda.

Kwa upande wake Mwenyekiti mteule wa tawi hilo Salawe Magembe amesema atahakikisha wanachama wenzake wanaimarisha tawi hilo.

Naye mchezaji wa zamani wa Pamba jiji Fc miaka ya 90 ambaye alikuwa mlinda mlango Madata Lubigisa ametoa rai kwa wapenda soka ndani ya Mkoa wa Mwanza kujitokeza kwa wingi katika tamasha la Pamba Day katika msimu huu 2024-2025.

“Nimefurahi mlivyo hamasika na timu yenu ya Wana Kawekamo TP Lindanda,Pamba Jiji FC ufunguzi wa tawi hili uwe msingi bora wa kupanga mikakati ya kuipa maendeleo timu yenu,”alisema Mdata

SOMA: RC Malima aipiga tafu Pamba FC

Kampeni hiyo inayoendelea katika wilaya zote za mkoa wa Mwanza huku ikihamasisha wakazi wa mkoa huo na maeneo jirani kuendelea kununua tiketi kwaajili ya tamasha la Pamba day litakalofanyika  Agosti 10,2024 katika uwanja wa CCM Kirumba