TANECU Mtwara yatakiwa kuongeza kasi uzalishaji korosho

CHAMA Kikuu cha Ushirika cha Tandahimba Newala Cooperative Union Limited (TANECU) mkoani Mtwara kimetakiwa kuongeza uzalishaji wa zao la Korosho ili kuendana na kasi ya ushindani wa zao hilo.
Akizungumza leo mkoani hapa katika Mkutano Mkuu wa 28 wa TANECU kwa mwaka 2023-2024 uliofanyika Halmashauri ya Mji Newala, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Ahmed Abbas amesema uzalishaji wa zao hilo haukuridhisha katika msimu huo hivyo C=chama hicho kijipange kuhakikisha kunakuwa na uzalishaji wenye tija katika msimu ujao.
Amesema uzalishaji wa korosho kitaifa kwa msimu huo ulikuwa ni tani 187,000.3 sawa na asilimia 67 ya lengo la kuzalisha tani 280,000 ambapo kwa Mkoa wa Mtwara ambao ndio unaongoza kwa uzalishaji wa korosho nchini, ulizalisha tani 99,000 zenye thamani ya Sh bilioni 176.3 sawa na asilimia 53.0.
Aidha TANECU kupitia msimu huo kilizalisha tani 33,500 sawa na asilimia 34.0 ya uzalishaji huo wa Mkoa wa Mtwara “Siyo wastani mzuri sana kwa TANECU tunayoifahamu mkutano huu utoke na mikakati ya namna ya kujipanga kuongeza uzalishaji huku, mkikumbuka tumeelekezwa na Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwa ifikapo mwaka 2025 kama Taifa tuwe tumefikisha uzalishaji wa tani laki 700,000”,
Kwa upande wake aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi cha (CCM) Mkoa wa Mtwara Yusuf Nannila amewasihi wanachama wa chama kikuu hicho kuwa wautambue uongozi wao huo na pale panapotokea changamoto yoyote ya kiutendaji wasiwahukumu tu na badala yake wawashauri ili Ushirika huo uweze kuimarika.
Aidha, watambue kwamba wanapofanya kazi hizo za Ushirika watambue kuwa Chama hicho kinawaangalia na kinawapenda lakini pia TANECU iwasikilize wanachama wake hao kwani ndiyo Ushirika wenyewe kinyume na hapo watauboma Ushirika huo.
Mwenyekiti wa Chama Kikuu Ushirika cha (CORECU Limited) kilichopo mkoani Pwani Mussa Hemed amesema kuwepo kwa Ushirika huo ni mafanikio makubwa kwa wanachama hao hivyo wasimame kwa pamoja ili kuhakikisha ushirika huo unasimama kwa manufaa ya tasnia hiyo ya Korosho na korosho jicho lake lote Nchi mzima liko Kusini ambako ni Mkoa huo wa Mtwara.
Mwenyekiti TANECU, Karim Chipola amesema yale yote yaliyoagizwa kupitia mkutano huo wameyapokea vizuri na kuahidi kuyafanyia kazi kikamilifu hasa suala la kuongeza uzalishaji wa zao hilo ambapo watazidi kuendelea kutoa elimu kwa wanachama/wakulima wao juu ya kufanya maandalizi mazuri katika mashamba yao.
Baadhi ya wanachama wa mkutano huo/wakulima akiwemo Ismail Ahmadi kutoka Chama cha Msingi cha Mitondi ‘B’ kilichopo Wilayani Tandahimba (AMCOS) “Kwa msimu wa korosho mwaka huu 2023/24 upo uwezekano mkubwa wa kuongezeka kwa uzalishaji kwasababu pembejeo za ruzuku iliyotolewa bure na Serikali imefika kwa wakati”,