Tanga Uwasa, EACOP kuboresha upatikanaji maji Muheza, Tanga

Tanga Uwasa, EACOP kuboresha upatikanaji maji Muheza, Tanga

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Tanga imeingia mkataba na  kampuni  inayosimamia ujenzi wa Bomba la mafuta (EACOP) wenye thamani ya Sh bilioni 3.1 ili kuboresha upatikanaji wa huduma ya maji kwa wilaya za Muheza na Tanga.

Akiongea kwenye hafla ya utiaji Saini mkataba huo Waziri wa Afya Ummi Mwalimu amesema kuwa mkataba huo unakwenda kusaidia kutatua changamoto ya upatikanaji wa huduma ya maji kwenye maeneo ambayo yalikuwa na uhitaji mkubwa wa huduma hiyo.

“Hii ndio tunaita kurudisha kwa jamii kwani wananchi wengi wanakwenda kunufaika na Mradi wa bomba lakini na kupata fursa ya huduma ya maji safi na salama,”amesema Waziri Ummy.

Advertisement

Mkurugenzi wa Tanga UWASA mhandisi Geofrey Hilly amesema kuwa fedha hizo zitakwenda kutekeleza miradi miwili ya maji huku zaidi ya wananchi 30,000 wakiufaika na huduma hiyo.

Msimamizi wa ujenzi kituo cha Tanga kutoka shirika la EACOP  Jerome Betat amesema mradi huo ni sehemu ya kurudisha kwa jamii iliyopo karibu na maeneo ya mradi.