Tanroads Shinyanga yaanza ukarabati makaravati

WAKALA ya Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Shinyanga imeanza matengenezo ya barabara na makaravati kwenye maeneo korofi yenye kilomita 70.49 kutoka Mwabomba hadi Ulowa.

Akizungumza Julai 17, 2023 Meneja wa wakala huo, Mhandisi Mibara Ndirimbi ambapo amesema matengenezo kwa ujumla yanatumia takribani Sh milioni 329.

Advertisement

“Kazi zitakazo fanyika ni kuinua matuta na kujenga makaravati maeneo korofi kumwaga changarawe na kuchonga mitaro katika Barabara ya Mwambomba Bugomba A, Bulungwa, Butibu hadi Ulowa.”alisema Ndirimbi

Mhandisi Ndirimbi alisema kipindi cha mvua maji yalikuwa yanakata barabara nakuleta usumbufu kwa wananchi ambapo kiangazi wameamua kuzikarabati ili zisiweze kuleta changamoto ya kutopitika vizuri tena.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Fly Construction inayotekeleza ujenzi huo Idd Iyombe aliishukuru serikali baada ya kutangazwa tenda nakuomba kisha kuchaguliwa na Barabara hiyo ilikuwa na changamoto ya maji kujaa juu ya daraja na kusababisha wananchi kushindwa kusafiri kupata huduma hasa kipindi cha mvua.

Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Bugomba ‘A’ Timothy Sasemi na Julieth Magadula wamesema ubovu wa barabara ulisababisha kushindwa hata kwenda kupata huduma kwenye zahanati kipindi cha mvua na watoto kwenda shule.