Tanzania, Iran kushirikiana sekta michezo

SERIKALI kupitia Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imeingia makubaliano ya kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika sekta ya Michezo.

Makubaliano hayo yameingiwa leo Oktoba 19, Dar es Salaam kupitia Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dk. Damas Ndumbaro na Jamhuri ya Kiislam ya Iran ikiwakilishwa na Waziri wa Kilimo, Gholamreza Nouri.

SOMA: Kamati ya bunge yaipongeza wizara ya sanaa, utamaduni na michezo

Advertisement

Nchi hizo zinatarajia kushirikiana katika Utalii wa michezo, kubadilishana wataalamu pamoja na kupeana uzoefu katika miundombinu ya michezo.

Hafla hiyo imehudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mahmood Thabit Kombo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa pamoja na wataalam wengine kutoka wizara hizo.