Tanzania kuingia ramani ya dunia uzalishaji wa dawa

SERIKALI imetangaza rasmi mwelekeo mpya wa kimkakati wa kuharakisha ujenzi wa viwanda vya dawa na bidhaa za afya nchini kwa lengo la kuimarisha usalama wa afya wa taifa, kupunguza utegemezi wa uagizaji wa dawa na kuiweka Tanzania kwenye ramani ya uzalishaji wa dawa Afrika na duniani.

Akizungumza katika kikao cha wazalishaji wa dawa na bidhaa za afya nchini, Waziri wa Afya, Mohamed Mchengerwa amesema kuwa ujenzi wa viwanda vya dawa si mpango wa majaribio bali ni uamuzi wa kimkakati uliokwishaamuliwa na serikali.

“Ujenzi wa viwanda vya dawa nchini Tanzania si jaribio, ni mwelekeo wa kimkakati uliokwishaamuliwa na Serikali,” alisema Mchengerwa.

Alisisitiza kuwa usalama wa afya wa taifa hauwezi kujengwa kwa kutegemea uagizaji wa dawa pekee bali unahitaji uzalishaji wa ndani unaokidhi viwango vya kimataifa miongozo na kanuni zilizowekwa na Shirika la Afya Duniani (WHO-GMP) “WHO-GMP si anasa wala cheti cha mapambo ni pasipoti ya kuingia sokoni kimataifa,” alisisitiza.

Katika hotuba hiyo, waziri ameweka wazi kuwa changamoto ya Tanzania katika biashara ya kimataifa ya dawa si ukosefu wa soko, wataalamu au fursa, bali ni viwango.

Akinukuu takwimu za hivi karibuni, alisema kuwa mwaka 2023 Tanzania iliuza dawa nje ya nchi chini ya Dola milioni moja ikilinganishwa na Kenya iliyouza zaidi ya Dola milioni 140. “Hili si tatizo la soko ni tatizo la viwango,” alisema.

Alisema serikali tayari imeanzisha mfumo maalumu wa uharakishaji wa uwekezaji. “Tumeondoa urasimu wa maamuzi ya mizunguko mirefu. Mwekezaji mwenye nia ya dhati atapata majibu ya haraka, ya wazi na yanayotabirika,” alisema Mchengerwa.

Kwa mujibu wa waziri, tangazo la kwa ajili ya uwekezaji katika uzalishaji wa dawa na bidhaa za afya tayari limetolewa rasmi likiwa na lengo la kuvutia wawekezaji wa ndani na wa kimataifa, kuhamasisha ubia wa kimkakati na kuharakisha kufikiwa kwa viwango vya kimataifa. Mwisho wa kuwasilisha maombi ni Machi 2, mwakani.

Ametoa wito kwa wazalishaji wa ndani kuwekeza katika ubora, teknolojia na mifumo ya viwango, akisisitiza kuwa msaada wa serikali utaelekezwa kwa viwanda vinavyokidhi au vinavyoonesha mpango wa wazi wa kufikia viwango vya kimataifa.

Alisisitiza: “Hatutalinda uzalishaji kwa sababu ni wa ndani pekee, bali tutalinda uzalishaji wenye ubora unaokidhi viwango vya dunia”.

Aidha, ametoa onyo dhidi ya jitihada zozote za kuhujumu au kuchelewesha kwa makusudi ajenda ya maendeleo ya viwanda katika sekta ya dawa, akisisitiza kuwa ni ya taifa na si ya kikundi fulani.

Kwa waingizaji wa dawa, waziri alisema mabadiliko haya si tishio bali ni fursa ya kuingia katika uzalishaji wa ndani kupitia ubia, uhamishaji wa teknolojia na uwekezaji wa muda mrefu.

Aidha, ametoa wito kwa wawekezaji na taasisi za fedha kuchukua fursa ya uwekezaji katika viwanda vya dawa, akieleza kwamba sekta hiyo ina soko linalokua, lenye mahitaji makubwa na uungwaji mkono wa sera katika ngazi ya juu ya serikali.

Alisema Tanzania ipo tayari kuwa kitovu cha uzalishaji wa dawa barani Afrika akisisitiza: “Mwelekeo wa sera uko wazi, soko lipo na wakati wa kuamua ni sasa.”

Habari Zifananazo

One Comment

  1. ★彡[𝐍𝐄𝐄𝐃 𝐏𝐄𝐎𝐏𝐋𝐄 𝐅𝐎𝐑 𝐏𝐀𝐑𝐓 𝐓𝐈𝐌𝐄 𝐎𝐍𝐋𝐈𝐍𝐄 𝐖𝐎𝐑𝐊]彡★

    Start making cash right now… I get paid over $220 per hour working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my befst friend earns over $19,000 a month doing this and she convinced me to try. ift was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by visiting Following Link…

    𝐇𝐞𝐫𝐞 𝐢𝐬 𝐈 𝐬𝐭𝐚𝐫𝐭𝐞𝐝=========> https://bs786s.blogspot.com/

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button