WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema ifikapo mwishoni mwa mwaka huu, Tanzania itakuwa na Rada saba ikiwa ni kiwango kikubwa cha Rada katika nchi za Afrika Mashariki na Kati.
Akizungumza leo Oktoba 13, katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Kupunguza Madhara ya Maafa, jijini Mwanza, Majaliwa amesema hatua hiyo ni katika jitihada za serikali kufanya uwekezaji mkubwa katika sekta ya hali ya hewa.
SOMA: Majaliwa asimamisha kazi vigogo wawili Iringa
Amesema kuwa hatua hiyo ni mwendelezo Serikali za kufanya uwekezaji katika sekta ya hali ya hewa nchini kwa kufunga miundombinu ya kisasa ya hali hewa ili kuimarisha mifumo ya ufuatiliaji wa taarifa za hali ya hewa.
Tanzania kuwa na Rada saba ikiwa ni kiwango kikubwa cha Rada katika nchi za Afrika Mashariki na Kati-Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
📍Mwanza-Tanzania
🗓️Oktoba 13, 2024✅Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kupunguza Madhara ya Maafa. pic.twitter.com/5sbPLv9711
— Ofisi ya Waziri Mkuu (@TZWaziriMkuu) October 13, 2024