Tanzania mabingwa mchezo wa goli Feasssa 2024
TIMU ya Tanzania katika mchezo wa mpira wa goli imeendelea kuonesha ubabe baada ya kutwaa ubingwa mara nne kwenye mashindano ya FEASSSA 2024 yanayofanyika mji wa Mbale, nchini Uganda.
Mchezo huo ulizikutanisha timu zenye wanafunzi wenye uoni hafifu na ni moja ya michezo inayoshindaniwa katika mashindano hayo.
SOMA:Timu za Tanzania zagawa dozi Feasssa Uganda
Aidha, wanafunzi Elisha Innocent Musa pamoja Tumsifu lazaro Kitambuli wameshika nafasi ya kwanza ya wachezaji bora wa mchezo huo.