Timu za Tanzania zagawa dozi Feasssa Uganda
TIMU za Tanzania zinazoshiriki michuano ya shule za msingi na sekondari ya Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (FEASSSA) zimeendelea kung’ara kwa kugawa dozi kwa timu pinzani katika michezo mbalimbali inayofanyika mji wa Mbale nchini Uganda.
Michuano hiyo inayofanyika viwanja vya shule ya sekondari Bukedea mjini humo, Jumatano Agosti 21 timu ya soka ya wasichana ya Tanzania iliibuka kidedea kwa kuifunga Uganda mabao 5-0 huku timu ya wavulana ikichapa Kenya mabao 4-0.
SOMA: Tanzania yaichapa Uganda mashindano ya Feasssa
Katika mchezo wa mpira wa kikapu timu ya wasichana Tanzania imeibuka kidedea kwa kuifunga Kenya mabao 66- 62 huku mchezo wa wavu, timu ya wasichana Tanzania imeichapa Kenya seti 3-1.
SOMA: Balozi Simuli awapa neno vijana Watanzania
Pamoja na michezo hiyo, katika mchezo wa mpira wa mikono timu ya wasichana imeifunga Uganda mabao 20-15.