Balozi Simuli awapa neno vijana Watanzania

BALOZI wa Tanzania nchini Uganda, Meja Jenerali  Paul Simuli ametoa rai kwa vijana wote nchini Tanzania kushiriki michezo ili  kupata ajira na kujenga mahusiano na nchi nyingine.

Akizungumza leo Agosti 19, 2024 na wachezaji wa Tanzania wanaoshiriki mashindano ya 22 ya michezo ya shule za msingi na sekondari ya Nchi za Jumuiya za Afrika Mashariki (FEASSA) yanayofanyika nchini Uganda, Balozi Simuli amesema pamoja na michezo kujenga afya lakini inatoa fursa ya ajira.

“Mmekuja kwenye mashindano haya ni muhimu yanawapa furaha na kuwaunganisha pamoja  vijana wa Afrika Mashariki. Viongozi mtoe kipaumbele kwenye michezo ili tupate vijana mahiri kwa kuwa ni eneo pia linalotoa ajira kwa vijana,” amesema.

SOMA: Timu ya Tanzania yakabidhiwa Bendera FEASSA

Amewataka vijana wa Tanzania kujitokeza kwenye michezo kuanzia ngazi ya msingi hadi sekondari kwa kuwa  Rais Samia Suluhu Hassan amewekeza fedha nyingi kwenye michezo hivyo ni jukumu la watanzania kuonesha vipaji vyao na kuleta ushindi.

Timu hiyo leo imeshiriki maandamano kwenye ufunguzi wa michezo hiyo yanayofanyika katika viwanja vya Bukedea, mji wa Mbale nchini Uganda

Michezo hiyo inafunguliwa leo Agosti,18, 2024 na Rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museven huku timu ya mpira wa miguu ya Tanzania ikifungua michezo hiyo dhidi ya Uganda.

Habari Zifananazo

Back to top button