Tanzania yaichapa Uganda mashindano ya Feassa
TIMU ya soka wasichana kutoka Tanzania imeshinda mabao 2-0 katika mchezo wa mashindano ya 22 ya michezo ya shule za msingi na sekondari ya Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (FEASSSA).
Michuano hiyo imeanza leo Agosti 19, 2024 katika viwanja vya Amus Collage School nchini Uganda kwenye hatua ya makundi.
Kwa upande wa mpira wa kikapu 3×3 Tanzania imeichapa Kenya kwa vikapu 13-10 huku mchezo 5×5 Tanzania imepata vikapu 43-58 dhid ya mabingwa watetezi Uganda.
SOMA: Balozi Simuli awapa neno vijana Watanzania
Vilevile, mchezo wa mpira wa mikono Tanzania ilicheza na Uganda ambapo hadi mwisho wa mchezo hakuna timu iliyoona lango la mwenzake.
Aidha, mpira wa soka wavulana Tanzania ilianza kwa kuichapa timu Rwanda magoli 1-0 lakini hadi mchezo unaisha Tamzania 2-2