LINDI: Waziri Mkuu, kassim majaliwa amesema Tanzania inatarajiwa kuwa mwenyeji wa mkutano mkubwa wa kimataifa kwa ajili ya uhamasishaji wa matumizi ya nishati safi duniani.
Lengo ni kuunga mkono jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa kinara katika uhamasishaji wa matumizi ya nishati safi nchini na Afrika.
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo Desemba 31 wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Hamasa ya Matumizi ya Nishati Safi mkoani Lindi akiwataka watanzania kumuunga mkono Rais Samia kwa kutumia nishati safi ya kupikia.
Aidha, Majaliwa amezungumzia faida ya matumizi ya nishati safi ambayo ni gesi, umeme pamoja na makaa ya mawe. Amesema nishati safi inalinda afya ya Watanzania, kulinda mazingira dhidi ya ukataji wa miti pamoja na kutoa ulinzi kwenye nishati endelevu.