Tanzania mwenyeji mkutano wa mamlaka usimamizi wa usafiri

TANZANIA kupitia Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) imeteuliwa kuwa nchi mwenyeji kwenye wa Makutano wa saba (7) wa Kimataifa wa Jumuiya ya Mamlaka za Usimamizi wa Usafiri Majini Barani Afrika utakaofanyika kuanzia Novemba 29 hadi Desemba 10, 2024 jijini Dar es salaam.

Katika taarifa iliyotolewa na Waziri wa Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa ilisema lengo la mkutano huo ni kujadili masuala muhimu ya maendeleao ya udhibiti na usimamizi wa usalama wa usafiri majini hatani afrika.

Imesema kipaumbele kikiwa ni mustakabali wa usafiri wa majini ma kuongeza ushirikiano baina ya nchi na wanachama.

Advertisement

“Kauli mbiu ya mkutano huo ni ‘ Kuimarisha mustakabali wa sekta ya usafiri majini barani Afrika, ushirikianao katika teknolojia na ubunifu ili kupunguza hewa ukaa, kuimarisha usalama wa mazingira, na mazingira ya sekta ya usafiri majini kwa mustakabali endelevy”ameandika

Ameongeza kuwa mkutano utafunguliwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt Dotto Biteko na kuhudhuriwa na Katibu Mkuu wa shirika la Bahari Duniani, Bw Antonio Dominguez pamoja na wataalam wa usafiri majini, viongozi wa mamlaka za udhibiti wa usafiri kutoka nchi na wanachama wa umoja wa Afrika zipatazo 50 ambazo zina bahari.

Pia Waziri amesema mkutano huo utatatumika kama jukwaa muhimu katika kuwezesha wadau kushiriki katika majadiliano yanayogusa masuala ya teknolojia na ubunifu yenye kulenga katika kuimarisha usalama wa usafiri majini.

“Ushiriki wa Dominguez ni heshima kubwa kwa Tanzania hasa kipindi hiki tunapotekeleza sera ya Taifa ya uchumi wa Buluu ambapo kama nchi tumebainisha masuala ambayo serikali kwa kushirikiana na Wadau” amesema Waziri Biteko

Aidha amebainisha Tanzania itaendelea kutangaza fursa za kiuchumi zilizopo katika sekta ya usafiri kwa njia ya maji zinazohusiana na utumiaji wa rasilimali za habari na maziwa zitakazo saidia kuongeza uwezo wa serikali kuwa hudumia wananchin na kuwaletea maendeleo.

Ametoa wito kwa wadau wa sekta ya usafiri majini, wakiwemo wasafirishaji, wamiliki wa vyombo vya usafirishaji majini, wawakilishi wa mashirika ya kimataifa, viongozi wa serikali kujitokeza kwa wingi kuhudhuria mkutano huo muhimu.