Tanzania yaingia soko la hisa New York

LIFEZONE METALS, Kampuni mama ya Tembo Nickel leo Julai 6, 2023,imeanza kuuza hisa zake kwenye Soko la Hisa la New York (NYSE).

Lifezone Metals ilitangaza nia yake ya kuweka hisa zake NYSE Desemba 2022.

Taarifa iliyotolewa leo na Kampuni ya Tembo Nickel imesema kuwa mradi wa Kabanga Nickel ni moja kati ya miradi mikubwa duniani ya madini ya Nickel ya kiwango cha juu ambacho hakijaendelezwa.

Advertisement

Kwa kutumia teknolojia ya Hydromet waanzilishi wa kampuni ya Lifezone Metals, wameongoza njia, Kabanga itaendelezwa kwa namna ambayo itapunguza uzalishaji wa hewa ya ukaa na kwa gharama ndogo, kwa lengo la kutengeneza metali za betri zinazohitajika duniani.

Uhusiano kati ya Tanzania na Marekani ni wa muhimu, ambapo mwezi Machi, Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan alimkaribisha Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris.

Kikao chao kilichofanyika Dar es Salaam kilionesha ukuaji wa uhusiano wa kimkakati kati ya nchi hizi mbili na mchango mkubwa wa Tanzania kama nchi inayochipukia katika uzalishaji wa madini ya kimkakati.

5 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *