WAZIRI wa Madini ,Anthony Mavunde amesema Tanzania imejipanga kuteka soko la uuzaji wa madini ya kimkakati yanayozalisha nishati safi yanayohitajika duniani ikiwemo madini ya Graphite.
Kauli ya waziri Mavunde imekuja ikiwa wakati dunia inaelekea katika Mkutano wa Kimatiafa wa Mabadiliko ya Tabia ya nchi (COP29) unaotarajiwa kufanyika kuanzia Novemba 11 hadi 22 nchini Azerbaijan huku ajenda miongoni mwa ajenda ikiwa ni matumizi ya nishati safi.
Amesema Tanzania kuna miradi mikubwa ambayo wanakwenda kuitekeleza hivi karibuni.
SOMA: Tumuunge mkono Rais, matumizi ya Nishati Safi
Akizungumza leo wakati wa mjadala wa mafanikio ya serikali ya awamu ya sita katika uboreshaji wa sekta madini nchini uliofanyika kwa njia ya mtandao amesema ifikapo mwaka 2050 wanategemea kwamba mahitaji ya madini mkakati yatakuwa kwa asilimia 150 zaidi kwa mahitaji ambayo yako leo duniani.
“Na madini mengi ambayo yanahitaji duniani tanzania inayo, tanzania ina nickel, lithium, graphite na yote hayo yanahitajika kwajili ya nishati safi,”amesema.
SOMA: Chalamila atoa maelekezo matumizi nishati safi
Ameeleza kuwa kwasasa wanajipanga kuwa moja kati ya nchi kubwa za kwanza Africa zinazozalisha madini mkakati ambapo mahitaji yake duniani ni tani mil 6.5 kwa mwaka na uzalishaji wa dunia hivi sasa ni tani mil 1.2 .
“China inaongoza kutoa asilimia 64 ya uzalishaji wote wa graphite duniani.
Waziri Mavunde amesema kwa afrika nchi ya kwanza inayoongoza ni Madagascar kwa asilimia 13,ya pili ni msumbiji kwa asilimia 10, na ya tatu ni Tanzania ambayo ina asilimia 0.6.