Tanzania yakaribisha waangalizi 72 wa AU

DAR ES SALAAM: Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria, Eliakim Chacha Maswi, amekutana na ujumbe wa waangalizi wa uchaguzi Mkuu kutoka Umoja wa Afrika (African Union Election Observation Mission) jijini Dar es salaam Oktoba, 27 2025.

Ujumbe huo wenye waangalizi 72 kutoka nchi 31 za Afrika umeongozwa na mwenyekiti wao ambaye ni Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Botswana, Mokgweetsi Eric Keabetswe Masisi.

Aidha, Serikali ya Tanzania ilitoa mwaliko kwa ujumbe huo ili kuangalia na kushauri kuhusu hali ya uchaguzi katika hatua ya maandalizi, wakati wa uchaguzi na baada ya uchaguzi.

Katika majadiliano yao waangalizi hao walijikita katika nafasi ya Wizara ya Katiba na Sheria kwenye Uchaguzi Mkuu.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button