Tanzania yapiga hatua ustawi rasilimali watu

MAKAMU wa Rais, Dk Philip Mpango amesema Tanzania imepiga hatua kubwa katika kusimamia ustawi wa Rasilimali watu kwa kuimarisha sekta mbalimbali nchini zikiwemo sekta za elimu, afya na TEHAMA.

Mbali na sekta hizo, maeneo mengine ni uimarishaji wa sekta binafsi na sekta nyingine tanzu zinazochagiza ustawi wa rasilimali watu.

Dk Mpango ameyasema hayo leo Julai 25, 2023 wakati akifungua Mkutano wa Kimataifa wa Wakuu wa nchi za Afrika kuhusu ‘Rasilimali Watu’ katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa  Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais amesema Tanzania imefanikiwa kupiga hatua hizo shukrani kwa uboreshwaji wa miundombinu ya elimu, utoaji wa elimu bure, kuruhusu wanafunzi walizopata ujauzito kuendelea na masomo.

Hatua nyingine ni  pamoja na uimarishaji wa sekta ya afya, ikiwemo manunuzi ya mashine ya MRI, CT- Scan na kuboresha sekta ya mawasiliano.

Mkutano huo unafanyika kwa siku mbili mfulululizo, ambapo kesho

Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuungana na wakuu wa mataifa mbalimbali  Afrika pamoja na viongozi wengine kushiriki mkutano huo kesho (Jumatano) ambao unaochagizwa katika mitandao  ya kijamii kupitia ‘hashtag’ #InvestInPeople.

Habari Zifananazo

Back to top button