Tanzania yapongezwa mifumo utoaji huduma

TANZANIA imepongezwa kwa kupiga hatua chanya katika mwelekeo kuunganisha mifumo ya utoaji huduma ya malipo yasiyotumia pesa taslimu, na uundaji wa miundo ya jumla ya serikali katika ngazi zote za serikali unaongeza na kudhibiti mapato.

Lakini pia asasi za kiraia hutoa mchango muhimu katika kisogeza uelewa wa Wananchi juu ya masuala muhimu ya kimaendeleo katika kutetea rushwa au kupinga ukatili wa kijinsia, lakini pia kueleza serikali changamoto wanazokumbana nazo katika kuleta haki na usawa.

Pongezi hizo zimetolewa na Balozi wa Uswisi nchini Tanzania, Didier Chassot kwenye wa uzinduzi wa wiki ya Azaki inayofanyika Jijini Arusha na kukutanisha NGOs kutoka ndani na nje ya nchi.

Chassot amesema ukusanyaji wa fedha kwa kutumia mfumo huo unaotekelezwa na serikali umewezesha kuunganisha uundaji wa miundo ya jumla ya serikali katika ngazi zote za serikali na kupelekea ukusanyaji mapato kubwa mzuri sanjari teknolojia kukua.

“Kama tunataka twende mbele kidigitali lazima sasa Azaki twende na mifumo hii ya kidigitali ambazo zitaongeza ufanisi na uwazi katika upatikanaji wa data za NGOs ambayo ikitumiwa vema italeta manufaa zaidi”

Naye Doreen Dominic ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Sekta za Umma wa Benki ya Stanbic, itaendelea kuboresha huduma zao kidigitali sanjari na kuboresha maisha ya watanzania hususani vijana na wanawake katika kuwapatia maendeleo.

Huku, Mrajisi wa Asasi za Kiraia kutoka Zanzibar Ahmed Khalid Abdulla amezitaka asasi za kiraia kusaidia jamii katika kufikisha taarifa za matumizi sahihi ya kidijitali ili waweze kutumia kama dursa zilizopo katika kujikwamua kiuchumi na maendeleo endelevu.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button