Tanzania yashiriki mkakati kutokomeza magonjwa sugu

TANZANIA inashiriki kikao kazi cha Mfuko wa Dunia wa Kupambana na Ukimwi,  Kifua Kikuu na Malaria (Global Fund).
Kikao kilichoanza Novemba 28, 2022 katika makao makuu ya mfuko huo Geneva, Uswis.
Tanzania imewakilishwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Profesa Abel Makubi, Naibu Katibu Mkuu Tamisemi Dk Grace Magembe na Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Geneva, Hoyce Temu.
 Akizungumza na HabariLEO leo Desemba 2,2022 Profesa Makubi amesema lengo la kikao kazi hicho ni ni  kujadili hatua zilizofikiwa katika kutekeleza miradi ya miaka mitatu (2021-2023) ya Ukimwi, Kifua Kikuu, Malaria na Uimarishaji Mifumo ya Afya na pia kujiandaa kwa andiko jipya litakalotekelezwa kwa kipindi cha 2024 -2026.
Amesema andiko hilo pia  litalenga kuelekea kutokomeza magonjwa hayo mahsusi  kabla ya mwaka 2030 pamoja na kuimarisha mifumo ya afya na ubora wa huduma za afya.
Aidha, Profesa  Makubi alimeushukuru  Ubalozi wa Kudumu wa Umoja wa Taifa, Geneva kwa kusimamia vema masuala ya sekta ya afya nchini uswisi ambapo kuna mashirika mengi ya kimataifa yenye kujishughulisha na afya.

Habari Zifananazo

Back to top button