TARI yatoa bure mbegu za minazi

MTWARA; TAASISI ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) kituo cha Mikocheni jijini Dar es Salaam kimetekeleza agizo la Rais Dk Samia Suluhu Hassan la kutoa bure mbegu za minazi kwa wakulima wa mikoa ya Lindi na Mtwara.

Raisi Dk Samia alitoa agizo hilo mwaka 2023 akiwa kwenye ziara ya kikazi katika mikoa ya Lindi na Mtwara, ambapo alimuagiza Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe kuwapatia wakulima wa minazi mbegu za kisasa ili kuendeleza kilimo cha minazi nchini.

Mtafiti wa mbegu za minazi kutoka katika kituo cha TARI Mikocheni, Vidaha Mahava amesema kituo hicho kimeshatekeleza agizo hilo kwa kutoa miche ya Minazi 54,000 kwa wakulima wa Lindi na Miche 34,000 kwa wakulima wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara.

Mahava amesema hayo katika Halmashauri ya Mtwara wakati wa ziara ya watafiti kutoka TARI Mikocheni walifika kukagua kitalu cha minazi ambazo kimeanzishwa na kituo hicho kuendeleza teknolojia bora ya kilimo.

“Kitalu hiki kilianzishwa kufuatia agizo la Rais Samia Suluhu Hassan wakati wa ziara yake mikoa ya Kusini ambapo alimuagiza Waziri wa Kilimo kuwapatia mbegu za minazi wakulima wa minazi Mtwara na Lindi, ” amesema na kuongeza kuwa lengo la kitalu ni kuwafundisha wakulima kanuni bora za kilimo cha zao la minazi.

Habari Zifananazo

One Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button