Taswa Marathon kufanyika Desemba

Mbio za TASWA Mwambao Marathon zinazoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) ambazo awali zilikuwa zifanyike mwishoni mwa mwezi uliopita sasa zitafanyika Desemba 22 mwaka huu jijini Tanga.

Kabla ya mbio hizo pia kutafanyika mkutano mkuu wa TASWA asubuhi ya Desemba 21 mkoani humo ambapo mchana wa siku hiyohiyo kutafanyika kongamano la kitaalam kwa wanahabari wa michezo kujadili masuala mbalimbali ikiwemo nafasi ya wanahabari kuelekea Afcon mwaka 2027.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kaimu Katibu Mkuu wa TASWA, Imani Makongoro, TASWA Mwambao Marathon 2024 ni mbio maalum yenye lengo la kuhamasisha wanamichezo kutumia Nishati Safi ya kupikia ili kutunza mazingira na kumtua mama kuni kichwani na kusukuma mbele mkakati wa serikali wa kuhakikisha kuwa hadi kufikia mwaka 2034 asilimia 80 ya watanzania wawe wanatumia nishati safi ya kupikia.

Advertisement

“Kutokana na mazingira hayo, TASWA inakaribisha mashirika ya ndani nan je, taasisi, kampuni, watu binafsi, wadau wa mazingira na nishati safi ya kupikia kushirikiana nasi kufanikisha mbio hizi ambazo ni kilometa 21, km 10 na mbio za kujifurahisha (fun run) za km 5,” TASWA ilisema kwenye taarifa yake.

Pia, Chama hicho kiliongeza kuwa watakaokuwa tayari mbio hizo watatakiwa kujisajili kwa namba ya malipo ya Tigopesa 0777333110 jina likisoma TASWA Marathon ambapo ada ni sh 30000.

Aidha, taarifa hiyo ilitoa wito kwa wanachama wake wote wanaotaka kushirki mkutano wake mkuu kushiriki kulipia ada ya uanachama ya mwaka mmoja ambayo ni sh 30000 kupitia benki ya CRDB Yenye jina la akaunti inayosomeka kama Tanzania Sports Writers Association (TASWA).

Namba ya akaunti ya kuchangia ada ni, 013364115070o huku mwiosho wa kuthibitisha ushiriki na kulipa ada kuwa Novemba 25, 2024.