TAWA yajipanga kutekeleza maono ya serikali

MOROGORO: MAMLAKA ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) imeipongeza Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuwezesha utoaji vibali vya kuajiri askari wa wanyamapori takribani 551 kwa mwaka wa fedha 2025/26.
Kaimu Kamishna wa Uhifadhi, Mlage Yussuf Kabange amesema hayo kwenye ziara ya wajumbe wa Bodi ya Nne ya Mamlaka hiyo ilipotembelea Makao makuu wa Tawa kwa muda wa siku mbili mjini Morogoro.
Bodi ya wakurugenzi hiyo inaongozwa na Mwenyekiti wake Meja Jenerali Mstaafu , Hamis Semfuko, ambapo pia aliwavisha vyeo vya kijeshi Makamishna wa Uhifadhi 13 katika hafla ya Kijeshi iliyofanyika katika Ofisi za TAWA Makao Makuu, Mkoani Morogoro.

Hivyo askari hao wataenda kuongeza nguvu katika uzimamizi wa ulinzi wa rasilimali wanyamapori.
“Maono ya bodi ya nne kwa kifupi tumeambiwa inataka kuiona TAWA inapaa na kuwa na ubora wa viwango vya utendaji kazi katika kazi za uhifadhi, kazi za utalii , kuvutia wawekezaji kushirikisha wananchi katika viwango vyote “amesema Kabange.
Kabange amesema utokana na malekezo ya Serikali, Waziri pamoja na bodi hiyo na maono yake ya kuiona Tawa inapaa, Menejimenti ya Mamlaka hiyo imejipanga katika utendaji kazi wake kwa ufanisi mkubwa.

Naye Naibu Kamishna wa Uhifadhi anayeshughulikia Kurugenzi ya Huduma za Shirika, Maarufu Thabit Mkwaya, amesema katika siku za hivi karibuni Mamlaka hiyo imepata askari wapya 296 .
Mkwaya amesema askari hao wanaenda kuongeza tija kwenye utendaji kazi wa Mamlaka na kwamba viongozi waliovalishwa na kupandishwa vyeo wao wanakwenda kwenye ngazi za kanda kwa maana ya viongozi wa kanda za Tawa.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi , Semfuko amewapongeza Makamishna kwa kuaminiwa na Bodi ya Wakurugenzi na kuteuliwa nafasi hizo katika maeneo mbalimbali ya usimamizi.

“Ninawapongeza Makamishna wote 13 waliotunikiwa na kuvishwa vyeo, ni imani ya Bodi kuwa mnastahili vyeo hivyo, hongereni ,” amesema Mwenyekiti wa Bodi Semfuko.
Amewataka kwenda kutekeleza maelekezo ya Serikali na maono ya bodi ya nne kwa kuhakikisha Mamlaka hiyo inapaa katika viwango vyote vya utendaji kazi ikiwemo ushirikishaji wa jamii, usimamizi wa kazi za uhifadhi, kuendeleza utalii, kuongeza uwekezaji na ukusanyaji wa mapato.
“Tunataka tuone TAWA inapaa juu zaidi na nyinyi ndio moja ya vichocheo vya kufanya hivyo,” amesema Semfuko.

Pia amewataka Makamishna wa uhifadhi kwenda kufanya kazi kwa kushirikiana na Maafisa na Askari walio chini yao kwa kuzingatia miongozo iliyopo huku wakizingatia ubunifu, weledi, sheria na utu.
Katika hafla hiyo Makamishna wa Uhifadhi waliovishwa vyeo ni Makamishna Wasaidizi Waandamizi ni saba ambao ni Privatus Kasisi, Wilbright Munuo, Khadija Malongo, Mark Chuwa, Vicky Kamata, Omary Msangi na Orest Njau.

Kwa upande wa Makamishna Wasaidizi ni sita ambao ni Alphonce Mung’ong’o, Jackson Msaki, Suleiman Keraryo, Jovine Nachihangu, George Makheya na Rajabu Hochi.




Cash earning job to earns more than $700 per day. getting paid weekly more than $3500 or more simply doing easy work online. no special skills required for this job and regular earning from this are just awesome. all you need is 2 hrs a day for this job and earning are awesome. every person can get this by follow details here…
THIS→→→→ https://Www.FindJobs1.Site
I get paid over (90$ to 200$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $18000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
.
HERE——————————————⊃⫸ https://Www.Cash54.Com
I get paid over 220 Dollars per hour working from home with 2 kids at home. i never thought i’d be able to do it but my best friend earns over 15k a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life. This is what I do, check it out by Visiting Following Website…
.
More Details For Us→→→→→→→→→ https://Www.Payathome9.Com
I get paid over 220 Dollars per hour working from home with 2 kids at home. i never thought i’d be able to do it but my best friend earns over 15k a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life. This is what I do, check it out by Visiting Following Website……….
HERE→→→→→→→→→→→ http://Www.Work27.Info