TAWJA Marathon yanoga Arusha

ARUSHA; MBIO Maalumu zilizoandaliwa na Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA) zijulikanazo kama TAWJA Marathon zimefanyika leo jijini Arusha.
Katika mbio hizo upande wa Kilometa 21 mshindi kwa wanaume aliibuka Victor Joseph aliyetumia muda wa saa 1:24:44 na kwa wanawake Mwajuma Shabani aliyetumia muda wa saa 2:01:59. Pia kulikuwa na mbio za Kilometa 10 na Kilometa 5.

Mwenyekiti wa TAWJA, Jaji Barke Sehel amesema mbio hizo zilienda sambamba na nia ya kuunganisha nguvu pamoja katika kupinga ukatili wa kijinsia,
Amesema mbio hizo ni ishara ya kuanza maadhimisho ya jubilei ya miaka 25 ya TAWJA yanayoadhimishwa Jumatatu jijini Arusha kusherehekea utofauti na mshikamano katika usawa wa kijinsia .



