Tax afanya ziara chuo cha Diplomasia Indonesia

WAZIRI  wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Stergomena Tax ameendelea na ziara yake nchini Indonesia  na kutembelea chuo cha Diplomasia cha Indonesia.

Waziri Tax pamoja na ujumbe wake, walipokelewa chuoni hapo na Mkuu wa Chuo hicho, Mohammad Koba.

Kufuatia ziara hiyo, Tanzania na Indonesia zimekubaliana kuanzisha ushirikiano baina ya vyuo vya Kidiplomasia, ikiwa ni pamoja na kubadilishana uzoefu  katika maeneo mbalimbali ikiwemo uendeshaji wa chuo na Programu za mafunzo kwa Wanadiplomasia, na kubadilishama ujuzi kwa walimu na wanafunzi wa vyuo hivyo.

Habari Zifananazo

Back to top button