TCAA yajipambanua maadhimisho ICAD 2025

DAR ES SALAAM: MAMLAKA ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imeungana na mataifa mengine duniani kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Usafiri wa Anga (ICAD) 2025.

Akizungumza katika maadhimisho hayo, yaliyofanyika Makao Makuu ya TCAA , Banana Ukonga jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Mhandisi Furaha Sanga, alisema ICAD ni siku muhimu inayotambua mchango wa sekta ya anga katika maendeleo ya dunia, ikiwemo uchumi, biashara, utalii, mawasiliano na usalama.

Katika hafla hiyo pia bendera ya Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga Duniani (ICAO) ilipandishwa. Maadhimisho ya mwaka huu yanaongozwa na kauli mbiu: “Safe Skies & Sustainable Future for All” ikimaanisha ‘Anga Salama na Mustakabali Endelevu kwa Wote.’

Mhandisi Sanga alisema kauli mbiu hiyo inaendelea kuikumbusha sekta ya anga umuhimu wa kuimarisha usalama huku ikihakikisha ukuaji endelevu kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.

Amesema kutoa elimu kwa jamii ni hatua muhimu katika kukuza uelewa na ushirikiano baina ya wadau wa sekta ya anga. Kama sehemu ya maadhimisho ya ICAD, TCAA pia imetoa elimu kwa umma kupitia vyombo mbalimbali vya habari nchini.

Elimu hiyo imejikita katika masuala mbalimbali ikiwemo majukumu ya TCAA kama mdhibiti wa sekta ya anga, usalama na matumizi sahihi ya ndege nyuki (droni), haki za abiria wa usafiri wa anga  pamoja na fursa zilizopo katika taaluma za anga sambamba na kutangaza huduma zinazotolewa na Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC).

Mbali na hafla iliyofanyika  Makao Makuu, pia  vituo vyote 15 vya TCAA nchini vimeadhimisha ICAD kwa kufanya shughuli mbalimbali zikiwemo utoaji elimu, majadiliano na wadau wa anga, pamoja na kutembelea vituo vya Watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu .

Mhandisi Sanga amevipongeza vituo hivyo kwa ubunifu na ushiriki mkubwa, akisisitiza kuwa maadhimisho ya ICAD ni ya kitaifa na yanawahusu watumishi wote wa mamlaka.

Kwa upande wa watumishi wa TCAA, Mhandisi Sanga ametoa wito wa kuendelea kufanya kazi kwa weledi na uadilifu, sambamba na kukumbatia mabadiliko ya kiteknolojia ili kuendana na mahitaji ya sekta ya anga duniani.

Amesema TCAA itaendelea kuboresha mifumo, huduma na usimamizi wa sekta kwa kuzingatia viwango vya kimataifa, ikilenga kuimarisha viashiria vya usalama kama USOAP na SASO kutoka ICAO.

Ameshukuru wadau mbalimbali wakiwemo mashirika ya ndege, taasisi za serikali, marubani, wahandisi na washirika wa usalama wa anga kwa kuendelea kushirikiana na TCAA katika kuhakikisha anga la Tanzania linabaki salama na lenye ufanisi.

Amehitimisha kwa kuwatakia watumishi na wadau wote maadhimisho mema ya ICAD 2025, akisisitiza dhamira ya Mamlaka kuendeleza kauli mbiu ya mwaka huu: “Anga Salama na Mustakabali Endelevu kwa Wote’.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. Google provides awesome remote work opportunities, allowing me to earn $2000-$3000 weekly with just 2-4 hours of daily work. It’s been a game-changer, offering flexibility and reliable income. If you’re seeking a genuine way to earn online, don’t miss this chance. Start today and transform your life!
    .
    More Details For Us →→ http://www.big.income9.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button