TCRA waanzisha kampeni ulinzi mitandaoni

MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Kaskazini imeanzisha kampeni kuwahimiza Watanzania kujilinda dhidi ya uhalifu mitandaoni kwa lengo la kutengeneza mazingira salama na kufikia uchumi wa kidijiti.

Akizungumza leo Septemba 9, 2024 jijini Arusha, meneja wa TCRA kanda hiyo, Mhandisi Francis Mihayo amesema matumizi ya teknolojia yamekua yakiongezeka kwa kasi hivyo muhimu katika maisha ya kila siku mamlaka hiyo kutoa elimu matumizi bora ya mitandao kwa Watanzania.

Mhandisi Mihayo amesema watu wengi nchini hawana ujuzi wa kutosha wa matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii pamoja na namna ya kulinda usalama wao mtandaoni jambo linalowafanya kuwa hatarini kwa mashambulizi, ulaghai na pia matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii.

SOMA: Jengo litakalobadili mandhari Arusha mbioni

Amesema mamlaka hiyo kupitia Kitengo cha Mawasiliano na Mahusiano ya Umma (CPRU)  inatambua umuhimu wa kukuza elimu ya kidigitali na kuhamashisha ya fursa zilizopo kwa matumizi sahihi ya mitandao kwa wananchi wote kushiriki kisiasa katika kipindi cha chaguzi mbalimbali nchini.

Mhandisi Mihayo amesema TCRA inaungana na dunia katika kuadhimisha mwezi wa elimu ya usalama mtandaoni ambayo huadhimishwa kila mwaka mwezi Oktoba na kitaifa ilizinduliwa Dar es salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Dk Jabir Bakari kwa uzinduzi kabambe uliojulikana kwa jina la ‘’Ni rahisi sana’’ na kwa kanda ya kaskazini imezinduliwa jana na meneja wa mamlaka hiyo.

SOMA: Kanuni mpya TCRA kufaidisha watengeneza maudhui …

Amesema katika kipindi cha uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu ujao Watanzania wanapaswa kuwa makini na taarifa za mitandaoni kwani baadhi ya watu watatumia mitandao hiyo kutoa taarifa feki na kuzua taharuki.

Meneja huyo amesema TCRA imekuwa ikitoa elimu katika maeneo mbalimbali ya wazi kwa miaka mingi ingawa utoaji wa elimu umeendelea kuwa endelevu wakati wote na mabadiliko ya kasi ya teknolojia yamekua yakienda sambamba na ongezeko la vitendo vya ulaghai mitandaoni.

Habari Zifananazo

Back to top button