TCU yaongeza siku 5 udahili wa wanafunzi

DSM: TUME ya Vyuo Vikuu Tanzania ‘TCU’ imeongeza siku tano kwaajili ya udahili kwa muhula wanne kwa wanafunzi  shahada ya kwanza katika taasisi za elimu ya juu nchini kwa programu ambazo bado zina nafasi kwa mwaka wa masomo 2023/2024.

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani  Dar es Salaam, Katibu mtendaji TCU, Prof Charles Kihampa amesema waliotuma maombi kwa madirisha yote matatu ni wanafunzi  142,440  wakati uwezo wa vyuo kuchukua wanafunzi ni 187,840.

Alisema kati ya mwanafunzi  ambao walipata nafasi  ni wanafunzi 130, 116 ambao walikosa ni wanafunzi 12,324 kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo wengine kukosa sifa, wengine changamoto ya kutozingatia sifa stahiki,

Advertisement

Prof Charles Kihampa amesema TCU inawapa tahadhari wananchi kuepuka kutapeliwa na watu wanaojiita mawakala au washauri wanaodai wanatoa huduma ya jinsi ya kujiunga na vyuo vya elimu ya juu hapa nchini.

“Waombaji ambao wengine labda walisoma shule ambazo zinatumia mitaala ya nje, lakini pia wapo waliomaliza stashahada, lakini pia kuna wale ambao walijaribu programu moja lakini akashindwa kufanya vizuri au hakuangalia zile sifa mahususi.

Kwa hiyo hili dirisha la nne waombaji, tunaomba walitumie vizuri kwa kuingia kwenye vitabu maalum na mitandao kwaajili ya kuangalia programu ya vyuo mbalimbali” alisema.

Mwisho alimalizia kwa kuwakumbusha waombaji udahili wa shahada ya kwanza kuwa masuala yote yanayohusu udahili au kujithibitisha katika chuo  yawasilishwe moja kwa moja kwenye vyuo husika.

1 comments

Comments are closed.