Teknolojia kupewa nguvu Afrika

DAR ES SALAAM: TANZANIA ni miongoni mwa nchi za Afrika zinazotarajiwa kushiriki mkutano wa Africa Blockchain Festival 2026, utakaofanyika nchini Kenya kwa lengo la kubadilishana uzoefu kuhusu matumizi ya teknolojia katika kukuza uchumi wa kidijitali.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Tume ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICTC), mkutano huo utajadili matumizi ya Akili Bandia (AI), teknolojia ya blockchain na Big Data katika kuboresha huduma na kukuza biashara kadhalika na kushirikisha watu wasiopungua 3000.
Naye Mwanzilishi wa mkutano huo, Olubunmi Fabanwo amesema teknolojia ya blockchain inahitaji kuunganishwa na teknolojia nyingine, ikiwemo Akili Bandia, usalama wa mitandao, utambulisho wa kidijitali na mifumo ya malipo.Amesema hatua hiyo ni muhimu katika kuongeza matumizi ya teknolojia hizo na kuleta manufaa zaidi katika uchumi wa kidijitali.

Kwa Tanzania, mjadala huo unatoa fursa ya kuangalia namna ya kuimarisha miundombinu ya TEHAMA, kuongeza ujuzi na kukuza ubunifu wa kiteknolojia.Wakati huo huo, Benki Kuu ya Tanzania inaendelea kufuatilia maendeleo ya teknolojia za kifedha.



