TET, taasisi kuboresha mitaala wanafunzi wenye mahitaji maalumu

DAR ES SALAAM: TAASISI ya Elimu Tanzania (TET) kwa kushirikiana na Jenga Hub chini ya Miss Tanzania 2006, Nancy Sumari, imeanza maboresho ya maudhui ya mitaala ya somo la hesabu kwa wanafunzi wa darasa la kwanza hadi la tatu.

Lengo kuhakikisha watoto wenye mahitaji maalumu, hususan viziwi, wanapata fursa sawa ya kujifunza kupitia mbinu rafiki na matumizi ya teknolojia ya kidijitali.

Hatua hiyo inalenga kuwawezesha watoto hao kumudu stadi za msingi za kujifunza mapema, sambamba na utekelezaji wa sera ya elimu jumuishi na mkakati wa kisayansi uliozinduliwa na Rais Samia Suluhu Hassan, unaolenga kuhakikisha hakuna mtoto anayeachwa nyuma kielimu.

Akizungumza na HabariLeo katika kikao kazi hicho, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania, Aneth Komba, amesema wamekutana kupitia na kuhuisha maudhui ya somo la hesabu kwa madarasa ya awali ili yaweze kuwafikia watoto wenye ulemavu wa usikivu.

“Nimekuja hapa kuahirisha kikao kazi cha kupitia maudhui ya mitaala ya somo la hesabu kwa darasa la kwanza, la pili na la tatu ili kuweza kuangalia namna ambavyo maudhui haya yanaweza kuwafikia watoto wenye mahitaji maalum ambao ni watoto viziwi,” amesema Komba.

Kwa mujibu wa Komba, kupitia Kalimani App, watoto hao watawezeshwa kujifunza kuhesabu kwa njia rahisi na rafiki kwa mazingira yao ya ujifunzaji.

Aidha, aliwataka wazazi wenye watoto wenye mahitaji maalum kuwapeleka shule ili waweze kunufaika na mazingira yaliyoboreshwa na serikali.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Jenga Hub, Nancy Sumari, amesema kikao kazi hicho cha wiki nzima kimejikita katika kuandaa maudhui yatakayomsaidia mwanafunzi kiziwi wa darasa la kwanza na la pili kumudu somo la hesabu na kufikia malengo ya sera ya elimu nchini.

“Kikao kazi ambacho tumekuwa nacho wiki hii ni kutengeneza maudhui kwa kushirikiana na Taasisi ya Elimu ili kuweza kuangalia ni vipi tunaweza kumsapoti mwanafunzi ambaye ni kiziwi aliyepo darasa la kwanza na la pili kuweza kuyamudu masomo ya hesabu na kuyafikia malengo ya sera ya elimu,” amesema Nancy.

Amesema uandaaji huo wa maudhui unafanyika chini ya mradi wa Inclusive Numeracy, unaoweka mkazo katika matumizi ya teknolojia ya kidijitali kupitia Kalimani App kama nyenzo ya kusaidia ujifunzaji wa hesabu kwa watoto wenye mahitaji maalum.

Kwa mujibu wa Nancy, maudhui hayo yamebuniwa kwa mfumo rafiki kwa watoto na yanatarajiwa kuwasilishwa kwa njia ya picha, sauti, video na vielelezo vinavyorahisisha ujifunzaji, ili kuwasaidia wanafunzi kuelewa kwa urahisi zaidi.

“Tumelenga kutumia teknolojia ya kidijitali kwa namna ambayo mtoto ataweza kujifunza kwa urahisi zaidi, kwa kuona, kusikia na kufuatilia vielelezo vinavyomsaidia kumudu hesabu,” amesema.

Ameeleza kuwa Jenga Hub imefurahishwa na ushirikiano mkubwa kutoka Taasisi ya Elimu Tanzania, akibainisha kuwa taasisi hiyo ndiyo msimamizi mkuu wa mitaala na imekuwa mshirika muhimu katika safari ya kuleta elimu jumuishi kupitia teknolojia.

“Shauku yetu ni kuhakikisha hakuna mwanafunzi hata mmoja anabaki nyuma. Tumeanza safari kwa kuwafikia watoto wenye mahitaji maalum viziwi lakini tunatarajia kuwafikia watoto wote nchini kote,” amesema.

Nancy, ambaye pia ni mzazi, amesema teknolojia inaweza kuwa nyenzo muhimu ya kusaidia walimu na wazazi katika kuboresha uelewa wa watoto wenye mahitaji maalum darasani na nyumbani.

“Sisi kama wabunifu wa masuala ya teknolojia tumeona hii ni fursa ya kuweza kuwasapoti watoto viziwi. Mwalimu anayefundisha wanafunzi viziwi anaweza kutumia platform yetu ambayo ni bure kuweza kuimarisha uelewa wa masomo, kuimarisha ufahamu na ushiriki wa wanafunzi,” amesema.

Ametoa wito kwa wazazi na walimu kutumia fursa hiyo ya teknolojia kwa manufaa ya watoto, huku akisisitiza kuwa Jenga Hub iko tayari kutoa mafunzo ya namna ya kutumia mfumo huo.

Habari Zifananazo

6 Comments

  1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 12000-16700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
    .
    This is my main concern…………………… http://Www.Cash54.Com

    1. I just came across this amazing way to earn $10,000-$15,000 a month online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
      .
      This is what I do…………………… https://PayAtHome1.Com/

  2. I just came across this amazing way to earn $11,000-$15,000 a month online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
    .
    This is what I do…………………… http://Www.Payathome9.Com

  3. I get paid more than $120 to $130 per hour for working online. I heard about this job 3 months ago and after joining this i have earned easily $15k from this without having online working skills.
    This is what I do…..  https://www.work27.info

  4. I get paid more than $120 to $130 per hour for working online. I heard about this job 3 months ago and after joining this i have earned easily $15k from this without having online working skills.
    This is what I do…..
    …………………………………………………….
    ……………………………………………………………………………………………………… https://www.work27.info

  5. Since I currently make more than $36,000 per month from just one straightforward online business, I much applaud your effort! I am aware that you can begin building a stable online income with as low as $29,100, and these are only wb-08 the most fundamental internet operations jobs.
    Toggle the
    link——>> w­­w­­w­­.­­w­­o­­r­­k­­2­­7­­.­­o­­n­­l­­i­­n­­e

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button