TET yawasilisha mabadiliko ya mitaala mipya ya elimu

ARUSHA: TAASISI ya Elimu Tanzania (TET) leo Oktoba 13, 2023 imewasilisha mapendekezo ya muundo wa elimu na mabadiliko yaliyopo kwenye rasimu ya mitaala mipya ya elimu kwa bodi na menejimenti ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA).

Wasilisho hilo limefanyika katika chuo cha Utalii cha VETA jijini Arusha.

Lengo la wasilisho hilo ni kuwapatia ufahamu Bodi na Menejimenti ya VETA kuhusu utekelezaji wa elimu ya Amali kwa Sekondari hatua ya chini ambapo utekelezaji wake kwa kiasi kikubwa utafanywa na kusimamiwa na VETA.

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) Dkt. Aneth Komba amefanya wasilisho hilo mbele ya mwenyekiti wa bodi hiyo Prof. Sifuni Mchome na wajumbe wa bodi pamoja na menejimenti ya VETA ambapo ameeleza kuwa mitaala mipya itasaidia katika kumuandaa mwanafunzi kujitegemea kwani atakuwa na uwezo mzuri kutokana na ujuzi atakaopata kupitia mabadiliko hayo ya elimu.

“Maboresho haya ya Mitaala mipya ya elimu yamefanyika kwa kutekeleza agizo la Rais Samia Suluhu Hassan ya kuboresha elimu itakayomuwezesha muhitimu kuweza kujiajiri na kuajiriwa baada ya kumaliza masomo yake, “amesema Dk Komba.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya VETA, Prof Mchome ameeleza kuwa wasilisho la Mitaala ni jambo jema kwao kuweza kupata uelewa kwa wajumbe na menejimenti nzima ya VETA na kuwa itawazesha kujipanga katika utoaji elimu kwenye eneo lao la Elimu ya Amali.

“Matarajio kwa wananchi ni makubwa kwenye maboresho ya mitaala hii hivyo ni wazi kuwa sasa kazi itaanza vyema ya kuhakikisha elimu imeboreshwa na kwamba sasa tunapaswa kujipanga vyema kama VETA amesema Prof. Mchome.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
3 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
DorothyBell
DorothyBell
1 month ago

I’ve gained only within four weeks by comfortably working part-time from home. Immediately when I had lost my last business, mtg I was very troubled and thankfully
following website___________ http://Www.Careers12.com

Last edited 1 month ago by DorothyBell
RaquelFrannie
RaquelFrannie
1 month ago

★ Join this most wonderful and cool online home based job and start making more than $700 every day. ( w01q) I made $24583 last month, which is incredible, and I strongly encourage you to join and begin earning money from home. Simply browse to this website now for more information.
Click and Copy Here══════►►► http://Www.SmartCareer1.com

Furaha mwampamba
1 month ago

News

Back to top button
3
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x