TET yawasilisha rasimu ya mitaala mipya

DODOMA: TAASISI ya Elimu Tanzania (TET) leo Oktoba 3, 2023 imewasilisha Rasimu ya Mitaala mipya ya Elimu kwa Makatibu Tawala Wasaidizi Elimu na Maafisa Elimu wa Halmashauri zote nchini ili kuwajengea uelewa juu ya rasimu hizo katika kikao kilichofanyika jijini Dodoma.

Wasilisho hilo limefanywa na Mkurugenzi Mkuu wa TET, Dk. Aneth Komba ambaye ameelezea namna Mitaala hiyo mipya itakavyosaidia kumwandaa mwanafunzi kujitegemea na kupunguza changamoto ya ajira nchini.

Amesema, maboresho ya Mitaala yanatekeleza agizo la Rais Samia Suluhu Hassan ya kuboresha Elimu ili mhitimu aweze kujiajiri na kuajiriwa baada ya kumaliza masomo.

Sambamba na hilo, Dk. Komba amewaomba Maafisa Elimu kuondoa hofu juu ya mabadiliko hayo kwani yana lengo zuri la kumuandaa mwanafunzi kupata elimu ya kujitegemea na kuajiriwa.

Naye, Mkurugenzi wa Usimamizi wa Elimu TAMISEMI, Vicent Kayombo ameishukuru TET kwa kushiriki kikao hicho na kutoa mada hiyo muhimu kwa mustakabali wa Taifa na kuahidi kuendelea kuishirikisha TET kutoa elimu zaidi ya Mitaala mipya katika vikao mbalimbali vya wasimamizi wa elimu hapa nchini walio chini ya TAMISEMI.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
3 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Bertha
Bertha
2 months ago

I make up to $90 an hour working from my home. My story is that I quit working at Walmart to work online and with a little effort I easily bring in around $40h to $86h… Someone was good to me by sharing this link with me, so now i am hoping i could help someone else out there by sharing this link… 

Try it, you won’t regret it!….. http://Www.Smartcash1.com

Last edited 2 months ago by Bertha
money
money
2 months ago

Conference ya wapi Wataelewa:-
·    Hospitali (wapeni ugonjwa waumwe wakajadiliane)
·    Mama ntilie (wape njaa wakale)
·    Hotelini (tengeneza events tualike)
·    Kwenye Basi (wape hela tusafiri)
·    Nyumbani (mpe hele ajenge)
·    Msibani (hakikisheni wanakufa na wawe na mahusiano mema)
·    Kijiwe cha kahawa (wape hela waje kunywa kahawa)
·    Jeshini (itisha mafunzo maalumu)
·    Darasani (anzisheni elimu ya watu wazima)

Umelogwa eti?

Capture.JPG
money
money
2 months ago

Conference ya wapi Wataelewa:-
·    Hospitali (wapeni ugonjwa waumwe wakajadiliane)
·    Mama ntilie (wape njaa wakale)
·    Hotelini (tengeneza events tualike)
·    Kwenye Basi (wape hela tusafiri)
·    Nyumbani (mpe hele ajenge)
·    Msibani (hakikisheni wanakufa na wawe na mahusiano mema)
·    Kijiwe cha kahawa (wape hela waje kunywa kahawa)
·    Jeshini (itisha mafunzo maalumu)
·    Darasani (anzisheni elimu ya watu wazima)

Umelogwa eti?…

Capture1.JPG
Back to top button
3
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x