TFS, NBAA wapanda miti Pwani

PWANI: Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) kwa kushirikiana na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) wameendesha zoezi la upandaji miti 600 katika Hifadhi ya Mazingira Asilia ya Pugu Kazimzumbwi, Kisarawe, mkoani Pwani ikiwa ni sehemu ya kampeni ya kuimarisha uhifadhi wa misitu na kukuza utalii wa ndani.
Akiongoza zaidi ya wahasibu 400 walioungana katika zoezi hilo, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi na Mhasibu Mkuu wa TFS, CPA SACC Peter Mwakosya, amesema hatua hiyo inaonesha namna taasisi za umma zinavyoweza kuchukua jukumu la kulinda mazingira na kuhimiza matumizi ya nishati mbadala.
Mwakosya amesema sekta ya maliasili na utalii ina mchango mkubwa katika uchumi wa taifa hivyo kuhimiza upandaji miti hususan msimu wa mvua ni njia madhubuti ya kuongeza uoto asilia na kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi.

Zoezi hilo limeambatana na matembezi ya utalii wa miguu na michezo ya kujenga afya, ambapo washiriki walipata nafasi ya kuona mandhari ya juu ya hifadhi hiyo inayotoa mwonekano wa zaidi ya asilimia 90 ya Jiji la Dar es Salaam.
Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa NBAA, CPA Fredrick Msumali, amesema ziara kama hizo zimekuwa sehemu ya utamaduni wa bodi kwa lengo la kuhamasisha wanachama kutambua umuhimu wa kulinda rasilimali za taifa.
Msumali amesema mwaka huu washiriki wamepanda miti 600, kutembelea maeneo ya hifadhi, kushiriki michezo mbalimbali na kupanda miinuko yenye mandhari pana ya jiji, pamoja na kujaribu shughuli za utalii wa maji kama uendeshaji wa mitumbwi na uvuvi.
Hifadhi ya Pugu Kazimzumbwi ni miongoni mwa misitu kongwe barani Afrika, ikiwa na hazina ya bioanuwai, mandhari adimu na historia ndefu ya ikolojia ya ukanda wa pwani, na imeendelea kuwa kivutio kikubwa cha watalii wa ndani na nje.




Single Mom Reveals How She Earns $89k/Yr Working 10 Hrs/Week From Home. Tired of paycheck-to-paycheck living? Meet Kelly from New York—a regular mom who cracked the code to recession-proof income without selling a thing! Now,Big thanks …
.
Here is I started____________________ http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→→→→→→→ https://Www.Payathome9.Com